UDOGO WAKO SIO KIGEZO CHA WEWE KUTOKUFANYA MAKUBWA
" Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme." #Mithali 30:24-28. Mistari tuliyosoma hapo juu inaonyesha jinsi gani viumbe hawa wanne ni wadogo, hawana nguvu, ni dhaifu, hawana kiongozi ( mfalme) lakini wanaweza kufanya mambo makubwa. Kuna funzo kubwa hapa kwa wale ambao wanajiona ni wadogo, wanajiona ni dhaifu, wanajiona hawana nguvu na wanajiona hawana kiongozi wa kuwasimamia. Udogo au udhaifu ulionao sio kigezo cha kutofanya jambo unalotakiwa kufanya. Unaweza kufanya unachotakiwa kufanya hata kama unajiona una nguvu kidogo. Unaweza kufanya mambo makubwa. Usiruhusu udogo au udhaifu ulionao kuwa kikwazo kwako kuanza kufanya jambo. Hacha kuangalia udogo ulionao, hacha kuangalia udhai...