Mbona Basi Mnaifanya Migumu Mioyo Yenu?

“Mbona, basi mnaifanya migumu mioyo yenu, kama vile wale Wamisri, naye yule Farao, walivyoifanya mioyo yao?...” 1Samweli 6:6 Bwana Yesu Kristo asifiwe! Ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa kutupa kibali tena cha kuiona siku hii nyingine na wiki nyingine tena ya leo. Namshukuru mungu kwa wema na fadhili zake zinazotufuata siku zote za maisha yetu kila iitwapo leo. Leo ningependa kuongea na wewe ambaye umekuwa unafanya moyo wako kuwa mgumu na hutaki kuisikia sauti ya Mungu na kumpa Yesu maisha yako. Naongea pia na wewe ambaye umeanguka dhambini na umeshindwa kurudi kwa Yesu tena. Mbona unaufanya moyo wako kuwa mgumu? Mbona utaki kuokoka? Nini kinakuzuia kumpa Yesu maisha yako? Je ni mali au shughuli za dunia? Je ni wazazi, ndugu au mpenzi? Je unajiona bado wewe ni mdogo na unasema ngoja nile ujana kwanza, Yesu badae? Je dhambi zimekuzidia unaona kwamba huwezi kuziacha? Sijui sababu yako ni ipi ndugu yangu inayokufanya usimpe Yesu maisha yako. Wakati ni sasa wa kump...