Wewe Ni Raia Wa Mbinguni
Yohana 17:14-16 [ 14]Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. [15]Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. [16]Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Bwana Yesu Mfalme asifiwe! Nazidi kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kwenye maisha yetu ambazo hazikomi kila kukicha. Kila asubuhi fadhili za Mungu ni mpya kwetu. Ni jambo jema na la kupendeza kumshukuru Mungu kwa jinsi ambavyo anatupigania, kutulinda na kuturehemu kila siku na kila muda. Leo natumia nafasi hii kukukumbusha kwamba wewe ambaye umempa Yesu maisha yako, ni raia wa Mbinguni. Maneno tuliyosoma kwenye kitabu cha Yohana 17 hapo juu ni miongoni mwa maombi amabayo aliyafanya Bwana Yesu kabla ya kwenda msalabani. Ni maombi ambayo ndani yake yanatukumbusha kwamba sisi sio raia wa dunia, bali uraia wetu ni wa Mbinguni. Ukisoma mlango wa 17 wa kitabu cha Yohana utaona jinsi ambavyo Bwana Yesu alituombea k...